Uturuki: Marekani inaanzisha ''bahari ya damu''
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ameishambulia Marekani juu kwa kuunga mkonoikundi kuu la wakurdi wa Syria. Ameishutumu serikali ya Marekani kwa kuanzisha "bahari ya damu" kwa kushindwa kutambua kama waasi wajumbe wa chama cha Democratic Union (PYD) na vugu vugu lake linalomiliki silaha.
Chama cha PYD, ambacho Marekani inakitegemea katika vita dhidi ya wanamgambo wa Islamic State ndani ya Syria, ni kikundi kilichotengwa na PKK.
Kauli ya Bwana Erdogan wakati akikabiliwa na shinikizo za kumtaka aruhusu raia wa Syria 30,000 waliokwama kwenye mpaka wa Uturuki.
Wakimbizi hao walikimbia mashambulizi ya vikosi vya serikali ya Syria na washirika wake kutoka vikozi vya wapiganaji katika maeneo yanayodhibitiwa na waasi yanayouzingira mji wa kaskazini wa Aleppo.
Waziri wa mambo ya ndani wa Ufaransa anaeondoka madarakani, Laurent Fabius, Jumatano pia ameikosoa sera ya Marekani nchini Syria, akisema kuwa haieleweki na imechangia kukwamisha juhudi za kumalizika kwa vita. "hatuhisi kwamba kuna utashi imara ," alisema Fabius.