Friday, May 27, 2016

DADA WA BILIONEA MSUYA AUAWA KWA KUCHINJWA

,
DADA WA BILIONEA MSUYA AUAWA KWA KUCHINJWA
Mtumishi wa Wizara ya Fedha, Aneth Msuya (30) ambaye ni mdogo wa Bilionea Erasto Msuya, ameuawa kwa kuchinjwa nyumbani kwake eneo la Kigamboni jijini Dar Es Salaam.
Akizungumza na mwandishi wa habari hii kwa simu kutoka Mererani, mmoja wa ndugu wa familia hiyo, Shujaa Khamis, alithibitisha kuuawa kwa Aneth (pichani), lakini alikataa kuingia kwa undani.
“Ni kweli wamemchinja usiku wa kuamkia leo (jana) na hapa nipo kwenye msiba hapa nyumbani (Mererani) kwa baba. Tumeambiwa wamechukua Tv tu,” alisema.
Hata hivyo, Khamis alikataa kueleza lolote kama wana mashaka na mauaji hayo zaidi ya kuliomba Jeshi la Polisi nchini, kuchunguza kiini cha mauaji hayo na kuwasaka waliohusika.
Friday, May 27, 2016 Dada wa Bilionea Msuya auawa kwa kuchinjwa By Daniel Mjema, Mwananchi dmjema@mwananchi.co.tz Habari Magufuli asema mazito Rais John Magufuli jana alituma ujumbe mzito katika mapambano dhidi ya…


0 comments to “DADA WA BILIONEA MSUYA AUAWA KWA KUCHINJWA”

Post a Comment